YANGA VS AZAM NI VITA YA KUGOMBEA NAFASI YA PILI TAIFA LEO
Pazia la Ligi kuu Soka Tanzania bara
msimu wa mwaka 2017/2018 linafungwa Leo Kwa timu zote 16 kucheza katika mechi 8
zitakazoamua mustakabali wa timu zote kwenye ligi hiyo kubwa kabisa katika
ngazi ya vilabu hapa Tanzania.
Macho na masikio yatakua hasa katika
mechi itakayoamua mshindi wa pili lakini pia timu itakayoungana na Njombe Mji
kushuka daraja.
Azam FC Ikiwa na pointi 55 katika nafasi
ya pili itakuwa Mgeni wa Mabingwa wa Kihistoria wa ligi hiyo Yanga wanaoshika
nafasi ya tatu wakiwa na pointi 52 Kwa hali ilivyo Azam FC wanahitaji sare tu
kuweza kushika nafasi ya pili huku Yanga wao ambao siku za hivi karibuni
wamekuwa wakisua sua watahitaji ushindi ili kuweza kumaliza katika nafasi ya
pili.
Mechi ya awali baina ya timu hizo
ilimalizika Kwa Yanga kushinda Kwa bao 1-0 katika uwanja wa Azam Complex
Chamazi goli pekee la Gadiel Michael Mbaga.
Katika balaa la kushuka daraja Maji Maji
ya Songea ambayo itacheza dhidi ya Mabingwa Simba kwenye uwanja wao wa nyumbani
wanahitaji ushindi ili kusalia katika ligi hiyo wakiwa na pointi 23 point moja
juu ya Njombe Mji na Ili Maji Maji isalie ligi kuu msimu huu inatakiwa kuifunga
Simba Leo bao 5-0 Halafu waombee Ndanda yenye pointi 26 ipoteze mchezo wake
dhidi ya Stand United pale Mtwara.
No comments