MANCHESTER UNITED SASA NJIA NYEUPE KUMNASA BALE.

Manchester City wameshaondoka katika zile mbio za kumsajili nyota wa Real Madrid na shujaa wa mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu Gareth Bale. Hali ambayo inaashiria kuwa njia ni nyeupe sasa kwa Manchester United kumsajili.

Bale anaweza kuondoka Real Madrid baada ya kuonesha kutokua na furaha klabuni hapo hasa baada ya kocha Zinedine kumwanzisha benchi katika mchezo huo wa fainali ambao ambao baadae alikuja kuibuka shujaa kwa kupachika mabao mawili.

Rekodi mbaya ya majeraha kwa mshambuliaji huyo raia wa Wales inatajwa kuwa sababu ya kutokua chaguo la kwanza la Zidane katika kikosi chake lakini inaaminika anaweza kuwa msaada kwa Man ambao walimfukuzia katika kipindi cha usajili wa majira ya joto msimu uliopita.

Wawakilishi wa Bale watakua na mazungumzo na Real Madrid hivi karibuni huku Rais Florentino Perez akibaki bila uhakika kama kiwango cha Bale katika mchezo wa fainali kimemshawishi kusalia nae kikosini.

No comments

Powered by Blogger.