WAMBURA AIBUKIA MAHAKAMA KUU, SAKATA LAKE KUIBUKA UPYA

Mahakama kuu ya Tanzania, Dar  es Salaam imekubali maombi ya Michael Wambura kutaka marejeo ya hukumu yake dhidi ya kamati ya maadili ya Shirikisho la mpira wa miguu (TFF).

Wambura ambaye alikuwa Makamu  wa Rais wa Shirikisho hilo alihukumiwa kutojihusisha na soka maisha baada ya kukutwa na makosa matatu yakiwemo kulitia doa Shirikisho hilo.

Hukumu kwenye shauri namba 20/2018 imetolewa na jaji Wilfred  Ndyasobera baada ya kuridhia hoja za mawakili wa Wambura, Masumbuko Lamwai na Emmanuel Muga.

Maamuzi hayo yanatokana na maombi yaliyowasilishwa Mahakama kuu wiki mbili zilizopita yakiomba Mahakama imruhusu Wambura kufungua kesi ya msingi kuomba kutengua maamuzi ya kamati za TFF.

Mahakama imeamuru kesi ya msingi ifunguliwe siku 14 kuanzia leo.

No comments

Powered by Blogger.