MAKONDA AFURAHI KOMBE LA VPL KUBAKI DAR

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema amefurahishwa kwa kombe la ligi kuu ya Vodacom kwa mara nyingine kuendelea kubaki jijini hapa safari hii likichukuliwa na Simba.

Kabla ya Simba kuchukua ubingwa huo msimu huu Yanga ilichukua mara tatu mfululizo kabla yake ilikuwa Azam FC zote za Dar.

Makonda amesema anajisikia vizuri kuongoza mkoa ambao kila kitu ndipo kinapo anzia huku akifurahishwa zaidi na Simba kutwaa ubingwa.

Kiongozi huyo ameongeza hata kama ingetokea timu kutoka Arusha  imetwaa ubingwa Mrisho Gambo angejisikia vizuri au ingekuwa Mwanza John Mongela angefurahi pia lakini kwakua imetokea Dar lazima afurahishwe na hilo.

"Nafurahi kuona timu kutoka Dar ikitwaa ubingwa wa ligi, mimi ni mkuu wa mkoa kwahiyo napenda kuona mara zote Mkoa wangu ukifanya vizuri," alisema Makonda.

Kuhusu maandalizi ya mchezo wa kesho wa ligi kati ya Simba dhidi ya Kagera Sugar ambao mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli amesema usalama umeimarishwa vya kutosha akiwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi.

"Niwahakikishie usalama  mashabiki watakao jitokeza kesho, wajitokeze kwa wingi bila hofu yoyote kila kitu kipo sawa," alisema Makonda.

No comments

Powered by Blogger.