SPORTPESA YAIPA MAMILIONI YA UBINGWA SIMBA
Mabingwa wapya wa ligi kuu ya Vodacom timu ya Simba imekabidhiwa hundi ya sh milioni 100 na wadhamini wao kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa.
Hafla hiyo imefanyika mchana huu katika ofisi za SportPesa zilizopo Masaki ambapo Simba walipeleka kombe la ubingwa kwa wadhamini hao.
Kiasi hicho cha pesa kimetolewa na SportPesa kwa mujibu wa mkataba waliongia ambao unasema kila wanapotwaa ubingwa watapewa kitita hicho.
Hundi hiyo ilikabidhiwa na Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas iliyopokelewa na Kaimu Makamu wa Rais wa Simba, Idd Kajuna.
Nahodha wa Simba John Bocco 'Adebayor' alikabidhi kombe hilo kwa Mkurugenzi huyo wa SportPesa.
Mbali na Simba, SportPesa inazidhamini timu ya Yanga na Singida United ambazo zote zinashiriki ligi kuu.
Baada ya ligi kuu kumalizika Jumatatu wiki ijayo Wekundu hao wataelekea nchini Kenya kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup itakayoanza Juni 5.

![]() |
Nahodha wa Simba John Bocco 'Adebayor' alikabidhi kombe hilo kwa Mkurugenzi wa SportPesa |

No comments