AWADHI AKUBALI MZIKI WA NDANDA AKIRI WALISTAHILI KUFUNGWA
Nahodha wa timu ya Mwadui FC, Awadhi Juma amekiri
kuwa katika mchezo wa jana dhidi ya Ndanda FC walizidiwa kila idara na
walistahili kupoteza.
Mwadui ilikubali kipigo cha mabao 3-0 katika mchezo
uliofanyika katika uwanja wa Nangwanda Sijaona na kurejesha matumaini ya
kusalia kwenye ligi msimu ujao.
Kiungo huyo wa zamani wa Simba alisema wapinzani wao
walicheza vizuri hasa kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata mabao yote
matatu.
Awadhi aliongeza kuwa kipindi cha pili walijitahidi
kutulia na kutuliza presha ya Ndanda lakini walishindwa kupata bao hata kufutia
machozi.
"Ndanda walicheza vizuri na walistahili
kushinda mechi ya jana, tutajipanga katika mechi ya mwisho ya kufungia msimu
dhidi ya Njombe Mji," alisema Awadhi.
Katika mchezo wa jana mabao ya Ndanda yalifungwa na
nahodha Jacob Massawe, Mrisho Ngassa na Tibar John.
No comments