SIMBA YAKOMALIWA SONGEA, MAJIMAJI YASHUKA DARAJA RASMI
Mabingwa wa ligi kuu bara timu ya Simba imemaliza msimu wa ligi 2017/18 kwa kulazimishwa sare bao moja Majimaji ambayo nayo imeshuka daraja rasmi.
Matokeo hayo yameifanya Majimaji kiluungana na Njombe kwa ajili ya kushiriki ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Katika mchezo huo Simba ilitumia idadi kubwa ya wachezaji wa akiba ikiaacha nyota wake wa kikosi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya michuano ya SportPesa Super Cup wiki ijayo.
Mshambuliaji Marcel Kaheza ambaye tayari amejiunga na Simba aliifungia Majimaji bao hilo dakika ya sita kabla ya Haruna Niyonzima kusawazisha kwa mkwaju wa penati dakika ya 45.
Ndanda FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Stand United na kujihakikishia kusalia kwenye ligi msimu huu.
Matokeo ya mechi zote za ligi kuu zilizpigwa leo
Mtibwa Sugar 0-0 Mbeya City
Lipuli FC 1-2 Kagera Sugar
Prisons 1-0 Singida United
Ndanda 3-1 Stand United
Majimaji 1-1 Simba
Njombe Mji 0-2 Mwadui
Mbao FC 1-1 Ruvu Shooting

No comments