SALAH ATHIBITISHA ATAKUWEPO RUSSIA.
Baada ya kutolewa nje katika dakika ya 30 tu ya mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid juzi usiku kutokana na maumivu makali ya bega, wasiwasi zaidi ulitanda kuwa huenda Mo Salah akaikosa michuano ya kombe la dunia itakayoanza katikati ya mwezi ujao huko Urusi.
Kupitia mtandao wa kijamii wa twitter, Salah amewahikikishia mashabiki wake kwamba anajiamini kuwa atashiriki michuano hiyo.
"Ulikua usiku mgumu sana lakini mimi ni mpambanaji, pamoja na mashaka yote, nina uhakika nitakuwepo Russia " Inasema sehemu ya ujumbe huo wa nyota wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri.
Salah pia amewashukuru mashabiki kwa upendo akiamini utazidi kumuimarisha. "Upendo na sapoti yenu vitanipatia nguvu ninayoihitaji" Aliongeza Salah
No comments