NIGERIA KUMKOSA MOSES SIMON KOMBE LA DUNIA


Katika kinachoonekana kuwa pigo kubwa kwa timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles ni taarifa kuwa mshambuliaji wao Moses Simon hatokua sehemu ya kikosi kitakachoshiriki michuano ya kombe la dunia.
Winga huyo aliyekua msaada mkubwa kwa Nigeria katika hatua za kufuzu amekua akisumbuliwa na maumivu yaliyopelekea akosekane kwenye mazoezi ya jana Jumapili huko Port Harcout wakijiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Congo DR utakaochezwa leo.

Bado haijafahamika ni nani atakayeziba nafasi ya Moses katika michuano hiyo

No comments

Powered by Blogger.