MKUTANO MKUU WA YANGA MWEZI UJAYO

Mkutano mkuu wa klabu ya Yanga umepangwa kufanyika Juni 17 badala ya Mei 5 kama ilivyokuwa imepangwa kutokana na ratiba za kombe la Shirikisho Afrika kuwabana pamoja na mechi za ligi.

Kamati ya utendaji ya klabu hiyo, imekutana juzi Jumanne kujadili mkutano huo na kuazimia kuupeleka mbele mpaka mwezi ujao ili kuwapa nafasi ya kuiandaa timu kwenye michuano hiyo.

Katibu mkuu wa klabu hiyo, Boniface Mkwasa amesema wamekubaliana kuweka nguvu na akili zao kwenye michuano ya Afrika na ligi na mkutano huo umesogezwa hadi Juni 17.

"Mkutano mkuu ambao ulikuwa ufanyike Mei 5 umesogezwa mbele hadi Juni 17 ili kuipa nafasi timu kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

"Mei 6 sita tuna mechi dhidi ya Algiers kwahiyo tukifanya mkutano mkuu tutapoteza umakini kuelekea mchezo huu muhimu kwetu, "alisema Mkwasa.

Mkwasa amesema wataendelea kutoa taarifa mara kwa mara kwa wanachama zikiwemo ajenda kuelekea mkutano huo ambao utajadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya klabu hiyo.

No comments

Powered by Blogger.