LICHA YA VIPIGO NJOMBE MJI BADO WANAKOMAA MPAKA MWISHO

Timu ya Njombe Mji imesema haijakata tamaa ya kusalia kwenye ligi msimu ujao licha ya kupokea vipigo mfululizo ikiwa inaburuza mkia kwenye msimamo.

Vibonde hao juzi walikubali kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Singida United katika mchezo ambao ulizamisha matumaini yao ya kuendelea kubaki kwenye ligi.

Njombe imesalia na mechi tatu kumaliza ligi ikiwa na pointi 22 ambapo inahitaji kushinda mechi zote huku ikiombea timu nyingine zisifanye vizuri.

Katibu mkuu wa klabu hiyo, Obeid Mwakasungura amesema hawajakata tamaa na watajitahidi kuhakikisha wanashinda mechi zilizobaki pamoja na kuwaombea wengine kupoteza.

"Ligi bado haijaisha tuna mechi tatu  zimebaki tunajipanga kushinda halafu tutaangalia wengine wamefanya  nini," alisema Mwakasungura.

No comments

Powered by Blogger.