EL CLASICO HAKUNA MBABE, RONALDO NA MESSI WATUPIA
Usiku wa Jana "Dunia ilisimama" kupisha pambano la soka kati ya miamba miwili nchini Spain ambao ni mabingwa Barcelona na Mabingwa wa Ulaya Real Madrid mchezo ambao ulimalizika Kwa sare ya bao 2-2.
Dakika 10 tu Barcelona walishaliona lango la Real Madrid Kwa kufunga bao safi baada ya juhudi kubwa zilizofanywa na Sergi Roberto aliyepiga krosi iliyomkuta Luis Suarez kuunganisha na kufunga bao Hilo.
Dakika 5 baadae Cristiano Ronaldo aliweza kuirudisha Real Madrid mchezoni akifunga bao la kusawazisha bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
Kipindi cha Pili Real Madrid walimtoa Cristiano Ronaldo baada ya kuumia wakati alipofunga bao la kusawazisha na nafasi yake kuchukuliwa na Marco Asensio.
Dakika ya 52 Lionel Messi aliifungia Barcelona bao la pili lakini dakika ya 72 Gareth Bale aliirudisha tena Real Madrid mchezoni akifunga bao la kusawazisha katika mchezo uliotawaliwa na kadi nyingi ikiwemo kadi Nyekundu ya Sergi Roberto dakika ya 45 lakini Real Madrid walipata kadi 5 za njano huku Barcelona wakipata kadi 3.
Mchezo huo wa ligi kuu ya Soka nchini Spain ulikua ni wa kukamilisha Ratiba tu lakini pia Kulinda Heshima wakati huu Barcelona wakishatwaa ubingwa wa ligi msimu huu.

No comments