CAF YAPITISHA HATUA YA KWANZA YA UKAGUZI TANZANIA MICHUANO YA U17
Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) limeridhishwa na maandalizi ya fainali za vijana chini ya miaka 17 ambazo Tanzania itakuwa mwenyeji zitazofanyika mwakani.
CAF ilituma Wakaguzi wake hapa nchini waliokaa kwa siku nne kukagua miundombinu ya viwanja vitakavyotumika, viwanja vya mazoezi, hospitali na barabara kama vinakidhi vigezo.
Kiongozi wa timu ya Wakaguzi kutoka CAF, Junior Binyam ameishukuru na Shirikisho la mpira wa miguu (TFF) na Serikali kwa maandalizi waliyofanya kuelekea michuano.
"TFF na Serikali zimefanya kazi nzuri, kwa niaba ya CAF nichukue nafasi hii kuwapongeza, ukaguzi wa pili utafanyika baada ya ripoti hii ya kwanza kukamilika," alisema Binyam.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Leodiger Tenga kwa niaba ya Serikali amesema mashindano hayo yatakuwa mazuri na ya kusisimua kwa mujibu wa maandalizi watakayofanya.
"Serikali imejipanga vizuri kupokea michuano hii, juzi mlimsikia Rais wa nchi Dk. John Magufuli na Waziri Mkuu wakizungumzia kuhusu michuano hili wakionyesha tumejipanga vilivyo," alisema Tenga.
Michuano hiyo imepangwa kufanyika katika viwanja viwili ambavyo ni uwanja wa Taifa na Azam Complex vyote za Dar es Salaam.

No comments