BARCELONA KUKIPIGA SOUTH AFRICA WIKI IJAYO

Kama mipango itakamilika basi Mabingwa wa Spain Barcelona Tarehe 16 May 2018 watakua nchini Afrika Kusini kucheza mechi ya kirafiki na Mamelodi Sondowns ya huko katika kuazimisha miaka 100 ya kuzaliwa aliyekua raisi wa Afrika Kusini na Mpigania Uhuru wa Waafrika Nelson Mandela.

Mamelod Sundowns wameomba mechi hiyo na tayari chama cha soka nchino Afrika Kisini kilituma wawakilishi nchini Spain kuweza kukamilisha dili Hilo.

Aidha Sundowns waliomba Shirikisho la soka barani Afrika CAF kuahirisha mechi yao ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhhidi ya Horoya AC ya Guinea ili waweze kucheza mechi hiyo.

 Mchezo huo uliopangwa kufanyika katika uwanja wa Taifa wa Afrika Kusini utakua wa pili kwa Barcelona kucheza nchini Afrika Kusini baada ya kufanya hivyo pia mwaka 2007 ambapo Barcelona iliibuka na ushindi wa bao 2-1.

Mamelody Sundowns ni Mabingwa wa Afrika Kusini wakati Barcelona ni Mabingwa wa Spain timu zote hizo zikichukua mataji hayo wiki iliyopita.

No comments

Powered by Blogger.