AZAM YAINGIA KAMBINI KUJIWINDA NA MAJIMAJI
Azam FC imeingia kambini leo kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Majimaji utakaofanyika siku ya Ijumaa.
Azam itawakaribisha Wanalizombe hao kwenye uwanja wao wa Azam Complex wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Stand United mwishoni mwa juma.
Azam imerejea jana jijini Dar es Salaam kutoka mkoani Shinyanga ilipokubali kibali hicho na leo imeingia kambini kujiwinda na mtanange huo.
Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd amesema wanatarajia kupata ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wao kutokana na kuwa kwenye nafasi mbaya katika msimamo wa ligi.
"Kikosi kimeingia kambini leo kujiandaa na mchezo ujao wa ligi utakaopigwa kwenye uwanja wetu wa Azam Complex siku ya Ijumaa dhidi ya Majimaji.
"Tunafahamu mchezo utakuwa mgumu kwakua Majimaji wanahitaji pointi ili wajiweke nafasi nzuri kwenye msimamo lakini nasi tumejipanga vizuri kuwakabili," alisema Jaffer.

No comments