YONDANI,TSHISHIMBI NA CHIRWA KUWAKOSA WA ETHIOPIA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Mabingwa wa soka tanzania bara klabu ya Yanga itawakosa wachezaji wao wanne kuelekea katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Timu yaWolaitta Dicha SC ya Etthiopia 

Katika barua yake ya tarehe 3/04/2018, ambayo www.wapendasoka.com ina nakala yake,Shirikisho la Soka barani Afrika CAF limewaandikia Yanga sambamba na wapinzani wao kuhusu wachezaji kadhaa wa timu zao ambao hawapaswi kucheza kutokana na kupata kadi mbili za njeno kwenye mechi zao zilizopita

Kwa Upande wa Yanga, Kelvin Yondani, Papy KabambaTshishimbi, Obrey Chirwa na Said Juma Ali wametajwa kuwa hawatoruhusiwa kucheza kutokana na kadi hizo walizopata kwenye michezo ya awali.

Yanga itaingiwa uwanjani Jumamosi hii ya tarehe 7 Aprili 2018 kucheza dhidi ya Wahabeshi hao ambao wameivurumusha Zamaleck ya Misri kabla ya kufikia hatua hii. 

No comments

Powered by Blogger.