BAADA YA SHOO YA RONALDO JANA LEO NI ZAMU YA MESSI MABINGWA ULAYA

Magoli mawili aliyofunga Cristaino Ronaldo jana akiiwezesha klabu yake ya Real Madrid kutanguliza mguu mmoja ndani katika kufuzu kwa hatua ya nusu fainali katika ligi ya mabingwa Ulaya wakiibuka na ushindi wa bao 3-0 ugenini dhidi ya Juventus imekua gumzo katika groups mbali mbali za soka duniani na pengine jina lake ndilo limetajwa zaidi duniani baada ya kuonyesha kiwango alichoonyesha.
Michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya Robo fainali itaendelea tena leo kwa mechi mbili kupigwa katika viwanja viwili barani humo.
Liverpool watakua nyumbani katika uwanja wa Anfield kucheza dhidi ya manchester City katika moja kati ya mechi mbili za leo ikikutanisha timu zote kutoka katika ligi kuu ya England
Barcelona wao ambao ni vinara wa ligi kuu ya Spain hivi sasa watakua Nou Camp kumenyana na AS Roma toka Italia mechi zote hizo zikitarajiwa kuanza saa 4 kasorobo za usiku
Macho na masikio leo yatakua kwa Lionel Messi wengi wakitaka kuona atafanya nini kuweza kuzima kelele za mashabiki wa Ronaldo na pia kuwapa raha mashabiki wanaomuunga mkono.
No comments