YANGA MPYA BILA LWANDAMINA YAANZA NA SARE TAIFA

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Soka Tanzania bara Yanga wamepata sare ya bao 1-1 na Stand United katika mchezo wa ligi kuu Soka Tanzania bara katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo wa Leo ulikua wa kwanza Kwa Yanga ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki katika michuano ya kimataifa baada ya kuondokewa na kocha wake mkuu George Lwandamina aliyetimkia klabu ya Zesco ya Zambia.

Nahodha as zamani wa Yanga Shedrack Nsajigwa ndiye aliyeongoza Benchi la ufundi la Yanga Leo akikaimu kama kocha mkuu.
Papy Salita Kambale alitangulia kuifungia Singida United bao la kwanza dakika ya pili tu ya mchezo lakini Abdallah Shaibu aliisawazishia Yanga dakika ya mwisho ya Kipindi cha kwanza na kufanya mchezo kwenda mapumziko timu hizo zikiwa sare.

Kipindi cha Pili hakikua na mabadiliko ya matokeo na kufanya timu hizo kugawana pointi moja kila moja katika michezo yao yote msimu huu katika Ligi kuu Tanzania bara.

No comments

Powered by Blogger.