RONALDO AIPELEKA REAL MADRID NUSU FAINALI MABINGWA ULAYA 



Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amefanikiwa kuivusha timu yake kwenda katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya

Ronaldo alifunga bao pekee la Real Madrid katika mchezo huo ambao Real Madrid walikubali kichapo cha bao 3-1 ukiwa ni mchezo wa marudiano baada ya ule wa awali ambao Real Madrid walishinda bao 3-0 jijini Turin.

Penati waliyopata Real Madrid dakika ya mwisho kabisa ya Muda wa nyongeza baada ya Medhi Benatia kuonekana na mwamuzi  Michael Oliver akimsukuma Lucas Vasquez wa Real Madrid ndiyo iliyowapa Real Madrid Ahuweni baada ya kucheza dakika 90 wakiwa nyuma Kwa bao 3-0.

Wapenda Soka wengi duniani waliamini shughuli ingekua rahisi kwa Real Madrid kabla ya mechi hiyo lakini mambo yalibadilika baada ya Juventus kupata mabao matatu yaliyofungwa na Mario Mandzukic aliyefumga mabao mawili na Blaise Matuid.

Matokeo hayo yanawafanya Real Madrid kutinga hatua ya nusu fainali Kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3.

Katika mechi nyingine Bayern Munich ilienda sare ya bila kufungana na Sevilla hivyo Bayern kutinga nusu fainali kwa ushindi wa bao 2-1 walioupata katika mechi ya awali nchini Spain.

Orodha  ya timu zilizotinga hatua ya nusu fainali ambayo Ratiba yake itapangwa Ijumaa hii ni:-

Real Madrid (Spain)
Liverpool  (England)
As Roma (Italia)
Bayern Munich  (German)

No comments

Powered by Blogger.