VPL: KIPORO CHA SIMBA KINALIWA LEO NJOMBE
Tayari Simba walishafika maeneo hayo tangu ijumaa wakitumia siku mbili mjini Iringa na jana walikua Njombe kwa ajili ya mchezo wa leo utakaoanza majira ya saa 10 za jioni.
Simba inaongoza msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa na pointi 46 sawa na Yanga lakini Simba ina magoli mengi ya kufunga huku ikiwa pia na faida ya mchezo wa leo na kama itashinda basi dhahiri itakuwa imeanza kuwakimbia Yanga kabla ya pambano lao baadae mwezi huu.
Jonas Mkude aliyekua majeruhi anaendelea vyema na pengine akawepo katika kikosi cha leo kama Kocha ataridhika kumpanga wakati wachezaji wengine wote wakiwa katika hali njema kuelekea mchezo wa leo.
Upande wa Njombe wao tayari wameshafika pia mjini Njombe baada ya safari ndefu ya kutoka Shinyanga ambapo Ijumaa waliondoshwa kwenye michuano ya kombe la FA na wenyeji Stand United.
Njombe Mji wako katika hatari ya kushuka daraja wakiwa na pointi 18 tu mpaka sasa katika nafasi ya 15 ikiwa ni pointi mbili tu juu ya majimaji wanaoshika mkia.
No comments