UCL LEO: REAL MADRID NA JUVENTUS, WABABE WA MAN UNITED NA BAYERN MUNICH

Image result for UCL Juventus vs Real madrid today
Hatua ya Robo fainali katika ligi ya mabingwa barani Ulaya inaanza leo kwa mechi za mzunguko wa kwanza wa hatua hiyo huku miamba minne ikionyeshana nguvu katika viwanja viwili tofauti barani Ulaya.

Mabingwa mara mbili mfululizo wa michuano hiyo Real Madrid watakua ugenini Uwanja wa Alianzi maarufu kama Juventus Stadium kuwavaa Juventus ambao ni washindi wa pili wa michuano hiyo msimu Uliopita.

Real Madrid iliifunga Juventus bao 4-1 msimu uliopita na kutwaa taji la michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo na imetinga hatua hii baada ya kuitupa nje PSG wakati juventus wao wameiondosha mashindanoni Tottenham Hotspur.

Mechi Nyingine hii leo itakua ni kati ya Sevilla ambao wametinga hatua hii baada ya kuitandika Manchester United kwa bao 2-1 katika mechi za hatua ya 16 bora na leo watakua nyumbani kucheza dhidi ya Bayern Munich ambao wametinga Robo fainali baada ya kuitupa nje Besiktas.

Mechi zote hizi zitaanza majira ya saa 4 kasorobo ya Usiku kwa saa za Afrika Mashariki 

No comments

Powered by Blogger.