VALDERDE ATAJA SABABU ZA KUWAACHA BENCHI MESSI, SUAREZ


Meneja wa Barcelona, Ernesto Valverde ametetea maamuzi yake ya kufanya mabadiliko ya kikosi cha kwanza na kupelekea kulazimishwa sare ya mabao 2-2 Celta Vigo jana usiku.

Mabao ya Ousmane Dembele na Paco Alcacer yalitosha kuisawazishia Barca baada ya Jonny Otto na Iago Aspas kuifungia Celta Vigo huku Sergi Roberto alitolewa nje kwa kadi nyekundu.

Nyota Lionel Messi na Luis Suarez walianzia benchi katika mchezo huo wakati vinara hao wakicheza mechi 33 za La liga bila kupoteza.
 
Messi na Luis Suarez wote walianzia Benchi 
"Ni kweli tulifanya mabadiliko kadhaa katika kikosi, kuna wachezaji ambao hawatumiki sana wamecheza na wameonyesha uwezo mkubwa, hilo jambo zuri kwetu," alisema Valverde.

Barcelona itakutana na Sevilla katika mchezo wa fainali wa  Copa del Rey siku ya Jumamosi.

No comments

Powered by Blogger.