UJIPANGE VYEMA UNAPOKUTANA NA SIMBA, MBEYA CITY WALIZWA VIBAYA

Vinara wa ligi kuu Soka Tanzania bara wekundu wa Msimbazi Simba wameendelea kufurahia ushindi katika mechi zake wakiibuka na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Wagonga Nyundo wa jiji la Mbeya klabu ya Mbeya City.

Simba ambayo licha ya kuongoza ligi lakini ndiyo timu pekee ambayo haijafungwa mchezo wowote mpaka na kuwafanya sasa kufikisha pointi 55 katika nafasi ya kwanza zikiwa ni pointi 8 mbele ya mabingwa watetezi Yanga wanaoshika nafasi ya pili.

Emmanuel Okwi ambaye ni kinara wa kupachika mabao alitangulia kuipatia Simba bao la kwanza kabla ya Asante Kwasi hajaongeza bao la pili.

Dakika moja baada ya Simba kufunga bao la pili Mbeya City walizinduka na kurejesha bao moja likifungwa na Haruna Shamte kabla ya John Bocco hajaongeza bao la tatu dakika 1 baada ya Mbeya City kufunga bao hivyo kufanya mchezohuo kwenda mapumziko Simba Ikiwa mbele Kwa bao hizo 3-1.

Hakuna mabadiliko ya matokeo katika kipindi cha pili licha ya kosa kosa nyingi kutoka Kwa timu zote mbili na matokeo yakabaki kama yalivyo.

No comments

Powered by Blogger.