TANZANIA YAPANDA NAFASI 9 VIWANGO VYA UBORA DUNIANI, UJERUMANI YAKAMATA USUKANI

Ushindi wa bao 2-0 walioupata wachezaji wa Timu yetu ya Taifa ya Tanzania maarufu kama Taifa Stars dhidi ya Congo DR Imeisogeza nchi Kwa nafasi 9 katika viwango vya ubora wa Soka Duniani vilivyotangazwa Leo katika mtandao wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA.


Tanzania imeweza kupanda kutoka katika nafasi ya 146 mpaka nafasi ya 137 katika viwango hivyo ikichangiwa na matokeo mazuri katika michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa.

Ujerumani ambao ni mabingwa wa dunia wanashika nafasi ya kwanza Kwa Ubora duniani ikifuatiwa na Brazil kisha Ubelgiji wakati Tunisia wanashika nafasi ya 14 na ya kwanza Afrika.

No comments

Powered by Blogger.