UCL : BARCELONA YAENDELEA KUNUFAIKA NA MAGOLI YA KUJIFUNGA MSIMU HUU

Barcelona players celebrate after Daniele De Rossi's own goal put them 1-0 up with seven minutes remaining in the first half
Vinara wa ligi kuu Soka nchini Spain klabu ya Barcelona Jana usiku ilipata ushindi wa bao 4-1 katika mchezo wake wa hatua ya kwanza ya Robo fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya AS ROMA.


Ikiwa nyumbani Barcelona iliendelea kunufaika na magoli ya kujifunga baada ya kupata mabao  mawili ya Kujifunga katika ushindi huo wa jana.

Daniele De Rossi na Konstantinos Manolas wa AS Roma walijifunga katika mechi hiyo kuwafanya Barcelona kufikisha goli 5 msimu huu ambazo wamezipata baada ya timu pinzani kujifunga ikiwa ndiyo timu pekee ambayo imepata faida hiyo msimu huu katika ligi ya mabingwa Ulaya.

Gerard Oique na Luis Suarez nao walifunga bao moja kila moja kwa upande wa Barcelona huku Edin Dzeko akiifungia AS Roma bao pekee katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Nou Camp.
Lionel Messi was handed with a commemorative plaque to celebrate him reaching 100 Champions League goals last time out
Messi alikabidhiwa ngao maalumu ya kufikisha mabao 100 katika ligi ya mabingwa Ulaya
Matokeo hayo yanawapa Barcelona nafasi kubwa sana ya kutinga hatua ya nusu fainali watakapocheza mchezo wa marudiano wiki ijayo jijini Roma.

No comments

Powered by Blogger.