UBINGWA WA MANCHESTER CITY WAPONGEZWA KILA KONA

City won the Premier League in style and bounced back with victory at Tottenham on Saturday
Manchester City jana walitawazwa kuwa mabingwa wapya wa ligi kuu ya England baada ya majirani zao Manchester United kukubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa West Bromwich Albion katika mchezo uliopigwa jioni ya jana katika dimba la Old Trafford.

Manchester City ambao Juzi waliifunga Tottenham Hotspurbao 3-1 ni kama hawakutegemea kwamba jana wangetawazwa kuwa mabingwa kwakua watu wengi walijua kama Manchester United wangeibuka na ushindi katika mchezo wa jana hivyo Man City wangeendelea kusubiri lakini matokeo hayakua hivyo na kupelekea City kutawazwa mabingwa kutokana na kuwa na pointi nyingi ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yoyote kwa sasa hata kama watapoteza michezo yake yote mitano iliyobaki.

Manchester City ambao msimu huu wamekua na kiwango kizuri sana tangu ulipoanza msimu huu na hii imepelekea kuzoa pointi nyingi ikiwa ni pamoja na kuzifunga timu zote ilizokutana nazo ikipoteza mechi mbili tu za marudiano dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield na dhidi ya Manchester United katika dimba la Etihadi.

Ubingwa wa Manchester City umepongezwa na wapenda soka wengi duniani na wengi wakisifia juhudi kubwa zilizofanywa na Kocha Pep Guadiola ambaye ameifanya Manchester City kuwa na anina flani ya soka la kufurahisha wakitumia pasi nyingi na kushambulia kwa sana.
Pep Guardiola applauds Manchester City's travelling fans after their win against Tottenham
Katika msimu wake wa pili kocha Pep Guadiola maefanikiwa kuiongoza Manchester City kushinda makombe mawili lile la Carabao na hili la Ligi kuu ya England baada ya msimu uliopita kushindwa kupata kombe lolote na kumaliza katika nafasi ya 3. 

No comments

Powered by Blogger.