MBIO ZA UBINGWA VPL: BOCCO NA OKWI WAIWEKA PAZURI SIMBA

Safu ya Ushambuliaji ya Simba imeendelea kuonyesha umwamba wake baada ya kufunga mabao yote mawili Leo katika ushindi wa bao 2-0 walioupata Vinara hao wa Ligi kuu Soka Tanzania bara dhidi ya Tanzania Prisons.

Emmanuel Okwi na Nahodha John Bocco ndiyo Vinara wa upachikaji mabao katika kikosi hicho cha wana Msimbazi ambao wamedhamiria msimu huu kushinda ubingwa na ndiyo waliofunga mabao ya Simba Leo.

Mpaka Mapumziko Simba walikua tayari wanaongoza Kwa bao 1-0 lililifungwa na John Bocco dakika ya 35 ya mchezo baada ya kufanya mashambulizi ya Mara Kwa Mara langoni mwa Prisons.
Eliuter Mpepo akijaribu kutaka kumtoka Beki wa Simba Shomari Kapombe

Kipindi cha Pili kazi iliendelea Kwa vijana wa Msimbazi Kwa kutafuta bao lingine huku safu yake ya ulinzi ikionekana pia kuwa imara kutoruhusu bao lolote la kusawazisha wakati wakitafuta bao la pili na dakika ya 79 mshambuliaji Emmanuel Okwi alimtengenezea Bocco wakati akijiandaa kupiga beki wa Prisons alimfanyia madhambi na kuzaa penati ambayo ilifungwa vyema na Emmanuel Okwi.

Simba ambayo haijafungwa mchezo wowote tangu kuanza Kwa ligi ya msimu huu imefikisha sasa pointi 58 Ikiwa na magoli ya kufunga 57 katika nafasi ya kwanza ikiiacha Yanga inayoshika nafasi ya pili Kwa pointi 11.

No comments

Powered by Blogger.