MAKONDA MGENI RASMI SIMBA NA YANGA
Mkuu wa mkoa wa Dar es
Salaam Ndugu Paul Makonda atakua mgeni rasmi wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara utakaowakutanisha Simba na Yanga utakaochezwa Jumapili Aprili
29,2018 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
Ndugu Makonda
atawaongoza maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu watakaojitokeza kweye Uwanja
wa Taifa kushuhudia mchezo huo namba 178 utakaoanza saa 10 jioni.
Tayari tiketi za mchezo
huo zinaendelea kuuzwa ambapo VIP A ni shilingi 30,000,VIP B na C 20,000 na
Mzunguko(Jukwaa la rangi ya Chungwa,Kijani na Bluu) 7,000.
Tiketi zinapatikana
kupitia Selcom.
Katika mchezo huo Simba
wanaingia uwanjani wakiwa wanaongoza ligi baada ya kujikusanyia pointi 59
ikicheza michezo 25 wakati Yanga wana pointi 48 wakiwa nafasi ya pili baada ya
kucheza michezo 23.
No comments