AZAM, MAJIMAJI ZASHINDA VPL, STAND, KAGERA ZAVIMBIANA
Timu za Azam FC na Majimaji zimepata ushindi katika mechi zao za leo za ligi wakati Stand United na Kagera Sugar zikigawana pointi kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
Azam iliibuka na ushindi wa bao moja ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar mtanange uliopigwa na uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
Azam imepanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kufikisha pointi 49 ikiizidi Yanga alama moja lakini ipo mbele kwa mechi tatu.
Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na Shaban Idd Chilunda dakika ya 38 baada ya walinzi wa Mtibwa kuzombea kuondoa mpira wa kona uliopigwa na Ramadhan Singano.
Mshambuliji Marcel Bonaventure ameisaidia Majimaji kujitoa kwenye nafasi ya kushuka daraja baada ya kufunga mabao matatu 'hat trick' katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting.
Bonaventure amefikisha mabao 13 na amekuwa mchezaji wa tatu kufunga hat trick msimu huu baada ya Emmanuel Okwi na Obrey Chirwa.
Majimaji imefikisha pointi 23 ikipanda nafasi mbili hadi ya 14 ikisalia na mechi nne baada ya kushuka dimbani mara 26.
Matokeo yote ya mechi za ligi kuu Vodacom bara Leo

No comments