MADRID YAINYAMAZISHA BAYERN MUNICH KWAO
Mabingwa watetezi wa michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya Real Madrid wameanza vyema mechi zake za nusu fainali baada ya kuibuka na Ushindi wa bao 2-1 Ugenini dhidi ya Wenyeji Bayern Munich.
Ili kujihami zaidi na matokeo ya ugenini kocha Zenedine Zidane alianzisha kikosi chenye viungo wengi kuweza kukabiliana na mashambulizi ya Bayern Munich kitu ambacho alifanikiwa sana akiwaacha kwenye benchi washambuliaji wake Karim Benzema na Gareth Bale huku Luka Modric, Toni Kroos, Casamiro na Isco wote wakianza katika mechi hiyo iliyopigwa katika dimba la Alianz Arena.
Dakika ya 28 Joshua Kimmich alitangulia kuipatia Bayern Munich bao la kwanza Kwa shuti Kali kabla ya Marcelo hajaisawazishia Real Madrid na kufanya timu hizo kwendà Mapumziko zikiwa ni sare ya bao 1-1.
Kipindi cha Pili Real Madrid waliingia wakiwa na malengo mawili kwanza Kulinda wasifungwe na pili kujitahidi kupata bao la ushindi na wakafanikiwa kujipatia bao la pili dakika ya 57 baada ya kazi nzuri ya Lukas Vazquez kumtengenezea "pacha" wake Marco Asensio nae bila ajizi akauweka mpira kambani.
Bayern Munich licha ya kukosa nafasi nyingi za wazi katika mchezo huo lakini walipata pia pigo baada ya Arjen Roben kuumia na kutolewa nje dakika ya 10 tu ya mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Thiago Alcantara.

No comments