BEKI MWINGINE WA AZAM KUPELEKWA AFRIKA KUSINI
Mlinzi wa kati wa timu ya Azam FC, Yakub Mohammed
anatarajiwa kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi wa mguu wake
uliokuwa umevunjika.
Mwezi uliopita mlinzi mwingine Daniel Amoah
alipelekwa nchini humo kupata matibabu ya goti ambapo mpaka sasa anaendelea
kuuguza maumivu yake.
Yakub tayari ametolewa bendeji gumu (P.O.P) mguuni
kwake lakini Daktari wao Mwanandi Mwankemwa amesema mchezaji huyo anahitaji
uchunguzi kabla ya kuanza mazoezi mepesi.
Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd amesema mchezaji
ataondoka nchini Mei mosi kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi wa
jeraha lake.
"Yakub anatarajia kuondoka nchini Mei mosi
kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi wa mguu wake kwa mujibu wa ushauri
wa daktari wetu Mwanandi," alisema Jaffer.
Wakati huo huo kikosi cha Azam kimeomdoka leo jijini Dar es Salaam kuelekea Morogoro kwa
ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa siku ya Jumamosi.
No comments