EPL: MAN UNITED, LIVERPOOL NA MAN CITY ZOTE VICHEKO


Baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa ligi mbalimbali barani Ulaya ligi zimerejea wakati huu tukielekea katika mwisho wa msimu huu wa mwaka 2017/2018.


Nchini England jumla ya mechi 8 zilichezwa kwenye viwanja tofauti huku Manchester City, Manchester United na Liverpool zote zikizoa point tatu muhimu.

Liverpool wakiwa ugenini jijini London waliifunga Crystal Palace bao 2-1 mchezo ambao Liverpool walitangulia kufungwa.

Manchester United Ikiwa nyumbani Old Trafford iliifurumua Swansea Kwa kuifunga Kwa bao 2-0 magoli ya Romelu Lukaku na Alexis Sanchez.

Manchester City wao wameendelea na ushindi katika mechi zao wakishinda bao 3-1 dhidi ya Everton mchezo uliopigwa katika uwanja wa Goodson Park.

Newcastle United wakaibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Huddersfield wakati Leicester City wao waliibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Brighton.

Watford wao wakiwa nyumbani walilazimishwa sare ya bao 2-2 na Bournemouth wakati West Ham United wenyewe walizinduka na kushinda bao 3-0 huku West Brom wakiendelea kupoteza mechi zake Kwa kufungwa 2-1 na Burnley.

Leo Jumapili mechi mbili zitachezwa Stoke City dhidi ya Arsenal wakati Chelsea wataialika Spurs.

No comments

Powered by Blogger.