AZAM KURA HAZIJATOSHA YATUPWA NJE FA
Timu ya Azam imeondolewa kwenye michuano ya FA na Mtibwa Sugar kwa mikwaju ya penati 9-8 kwenye mchezo wa robo fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex.
Mtibwa imekuwa timu ya tatu kuingia nusu fainali baada ya Stand United iliyoitoa Njombe kwa bao moja na Polisi Tanzania ikitoa Tanzania Prisons kwa mabao 2-0.
Mchezo huo ulilazimika kwenda kwenye changamoto za penati baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika muda wa kawaida.
Azam ilicheza vizuri zaidi kipindi cha kwanza kwa kutengeneza nafasi lakini Mtibwa wao walikuwa bora kipindi cha pili huku wakionekana kujilinda kuliko kushambulia
Penati za Mtibwa zilifungwa na Hassan Dilunga, Ismail Muhesa, Stamili Mbonde, Nditi, Hassan Isihaka, Hassan Mganga, Salum Kihimbwa, Kasian Ponera, Dickson Daud wakati Henry Joseph akikosa mkwaju wake.
Wakati zile za Azam zilifungwa na
Himid Mao, Yahaya Zayd, Bruce Kangwa, Agrey Morris, Joseph Kimwaga, Joseph Mahundi, Salehe Abdallah na Salum Abubakar wakati Frank Dumayo na Abdallah Kheri wakipoteza mikwaju.
Kesho kutakuwa na mchezo mmoja wa kukamilisha robo fainali ya michuano ambapo Singida United itaikaribisha Yanga kwenye uwanja wa Namfua.
No comments