SIMBA NA YANGA SASA KUPIGWA APRIL 29


Mechi ya watani wa jadi baina ya Simba na Yanga katika mzunguko wa pili wa lala salama itapigwa tarehe 29 ya mwezi wa April katika uwanja wa taifa

Akiongea na waandishi wa Habari katika ofisi za TFF leo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya ligi, Boniface Wambura ametangaza mechi zote zilizokuwa tarehe zake hazijapangwa.

Ligi hiyo inayotoa mwakilishi katika michuano ya klabu bingwa inatarajiwa kumalizika mei 26 na kufuatiwa na fainali ya kombe la Fa ambae bingwa wake atashirki kombe la shikisho.

Mechi pekee zilizofanyiwa marekebisho ni zile ambazo zilihusisha Simba na Yanga kwa kuwa ratiba ziliingiliana kupisha michuano ya kimataifa alisema Wambura

Ratiba yote iliyofanyiwa marekebisho hii hapa


Njombe Mji vs Simba (3 Aprili)
Mbao FC vs Lipuli ( 6 Aprili )
Mwadui FC vs Majimaji ( 7Aprili )
Mtibwa Sugar vs Simba ( 9Aprili )
Yanga vs Singida United ( 11 April)
Simba vs Mbeya City ( 12 Aprili)

No comments

Powered by Blogger.