KOCHA WA DR CONGO AWATAJA SAMATA, MSUVA NA ULIMWENGU
Kocha wa timu ya Taifa
ya DR Congo, Ibenge Florent amesema haifahamu vizuri timu ya Tanzania lakini
wachezaji watatu ndio anawajua ambao ni nahodha Mbwana Samata, Simon Msuva na
Thomas Ulimwengu.
Kocha Ibenge amekiri
kuwa mchezo wa kesho dhidi ya Taifa Stars utakuwa mgumu na anatarajia kupata
upinzani mkubwa kutoka kwa wenyeji.
Ibenge ameongeza kuwa
moja ya sababu kuchagua kucheza na Stars ni kutokana na ukaribu pia Tanzania
ina wachezaji wengi vijana wenye vipaji ambao watawapa ushindani.
"Sijui vizuri
soka la Tanzania lakini nawajua Samata, Msuva na Ulimwengu lakini naamini kuna
wengine wazuri," alisema Ibenge.
Mchezo huo ambao
utapigwa kwenye uwanja wa Taifa utaanza saa 10 jioni.
No comments