MSUVA AANIKA FAIDA YA KUCHEZA SOKA LA KULIPWA


Winga wa timu ya Taifa ya Tanzania, Simon Msuva anayechezea Difaa El Jadida ya Morocco amesema kucheza soka la kulipwa kunatoa mchango mkubwa katika kukua kwa mpira wa nchi.


Nyota huyo wa zamani wa Yanga amesema uwepo wa wachezaji wanaotoka nje wakisaidina na wa ndani wanatengeneza muunganiko mzuri ambao ni faida kwa Stars.

Msuva na nahodha Mbwana Samata, Abdi Banda na Rashid Mandawa ndio wachezaji wa Stars wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Msuva amesema kuwa uwepo wao ndani ya kikosi hicho uliongeza chachu ya ushindi wa mabao 2-0 iliyopata Stars jana dhidi DR Congo katika mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Taifa.

"Kucheza soka la kulipwa nje ya nchi kuna faida kubwa kwanza kunaongeza kujiamini uwanjani kwakua unakutana na nyota mbalimbali mahiri hata kwetu limedhihirika hilo.

"Hata hizi mechi mbili za kirafiki dhidi ya Algeria na Congo zimetuongezea kitu kikubwa ambacho kitatusaidia sana kwenye michuano ijayo," alisema Msuva.

Msuva amegeuka lulu katika klabu ya Difaa kutokana na uwezo mkubwa wa kufunga mabao huku akiwahi kuchaguliwa mchezaji bora wa ligi hiyo.

No comments

Powered by Blogger.