KAMATI YA RUFAA KUMRUDISHIA WAMBURA UMAKAMU?
Sakata la kufungiwa Maisha Kwa makamu wa Rais wa TFF ndugu Michael Wambura limeingia hatua nyingine baada ya Leo kupewa barua ya wito wa kuhudhuria katika kamati ya Rufaa ya Shirikisho Hilo.
Nakala ya barua hiyo ambayo imesainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF ndugu Wilfried Kidao na www.wapendasoka.com kubahatika kuipata inaeleza kwamba kamati ya Rufaa na maadili itaketi katika kikao chake cha Tarehe 31 Machi 2018 siku ya Jumamosi saa 5 kamili asubuhi katika ofisi za Shirikisho hilo zilizopo Katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine kamati hiyo itasikiliza Rufaa iliyowasilishwa na Wambura kupinga maamuzi ya kamati ya Maadili iliyomfungia maisha kujihusisha na maswala ya soka pamoja na kumvua nafasi ya makamu wa Rais.
Aidha Wambura ametakiwa kwenda na vielelezo vya utetezi wake siku hiyo Ikiwa ni hatua ya mwisho ya kuweza kiendelea kulitumikia Shirikisho Hilo au kuachana kabisa na Soka.
No comments