MSHAMBULIAJI SAUDI ARABIA ATUA MAN UNITED

Mshambuliaji wa SAUDI ARABIA Mohammad Al-Sahlawi amekubaliwa kufanya Mazoezi na kikosi cha Manchester United chini ya kocha Jose Mourinho ili kujiweka vyema kabla ya kombe la dunia.

Mohammad mwenye miaka 31 ndiye mshambuliaji tegemezi wa Saudi Arabia ambaye Ana rekodi nzuri Kwa timu yake ya Taifa akiwa ameshafunga mabao 26 katika mechi 33 akiwa na timu yake ya Taifa.

Rais wa chama cha Soka cha Saudia aliandika  katika ukurasa wake wa Twitter kuhusu Mohammad kukubaliwa majaribio ya wiki tatu katika klabu ya Manchester United.

Kocha Jose Mourinho hajaonyesha nia yoyote ya kumsajili mchezaji huyo anayeichezea Al-Nassr ya Saudi Arabia lakini makubaliano yamefikiwa kutokana na sababu za kibiashara zaidi.

Saudi Arabia itafungua mechi za fainali ya kombe la dunia mwaka huu watakapocheza dhidi ya Wenyeji Russia

No comments

Powered by Blogger.