MAKOSA YA SAFU YA ULINZI YAIMALIZA STARS KWA ALGERIA
Makosa ya safu ya Ulinzi ya timu ya taifa ya Tanzania yani Taifa Stars yamepelekea kufungwa bao 4-1 na timu ya taifa ya Algeria katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopigwa huko nchini Algeria.
Mpaka Mapumziko tayari Taifa Stars ilikua nyuma kwa bao 2-1 magoli yote mawili tukifungwa kutokana na kutokua makini kwa wachezaji wetu hasa wale wa nafasi ya ulinzi ikiwa ni pamoja na Shomari Kapombe kujifunga wakati akiwa katika harakati za kuokoa mpira wa krosi.
Katika kipindi hicho cha Kwanza Simon Msuva ndiye aliyeipatia Taifa Stars goli pekee katika mchezo huo huku algeria wakiongeza mashambulizi na kupata mabao yao mawili zaidi kukamilisha ushindi huo
Magoli ya Algeria yalifungwa na BaghdadBounedjah aliyefunga mabao mawili, shomari kapombe bao la kujifunga na bao moja la carl Medjani.
Taifa Stars Jumanne ya wiki ijayo itacheza dhidi ya Congo DRC katika mchezo mwingine wakati huu wa mechi za kirafiki za mataifa mbali mbali.
No comments