GIGGS AANZA NA BAO 6-0 TIMU YA TAIFA YA WALES, BALE APIGA HAT-TRICK NA KUWEKA REKODI MPYA
Mechi hiyo ya kimataifa ya kirafiki imefanyika nchini China katika uwanja wa Guangxi sports Centre jijini Nanning China
Gareth Bale amefanikiwa kuweka rekodi katika mechi hiyo akifunga mabao matatu yani hat-trick kumfanya afikie mabao 29 na kumfanya mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Wales akiipita rekodi iliyowekwa na mkongwe Ian Rush ambaye alifunga mabao 28 huku Bale akifikisha rekodi hiyo katika mechi 69 tu alizoichezea Wales wakati Rush aliweka rekodi yake katika mechi 73.
magoli mengine katika mechi hiyo yalifungwa na Sam Vokes aliyefunga bao mbili na Harry Wilson aliyefunga bao moja.
No comments