WATU WALIA NA "MIKEKA", MAN CITY IKITUPWA NJE KOMBE LA FA.


Kuna msemo unapenda kutumiwa na wachambuzi wa Soka la kileo kwamba "Soka Halina Mwenyewe" na ndiyo hasa kilichodhihirika usiku huu katika uwanja wa DW  Wakati Wenyeji Wigan Athletic walipoifunga Manchester City bao 1-0.

Mechi hiyo ya mwisho katika hatua ya tano ya michuano ya Kombe la chama cha Soka nchini England maarufu kama FA CUP ambayo inaipa Sasa Wigan nafasi ya kutinga hatua ya Robo fainali wakipangwa kucheza na Southampton.

Goli pekee lililowazamisha Manchester City Leo lilifungwa dakika ya 79 na mshambuliaji Will Grigg ambaye amefikisha magoli 7 katika michuano hiyo msimu huu. Huku Manchester City wakiendelea rekodi mbovu dhidi ya Wigan.

Manchester City walicheza kipindi chote cha pili wakiwa pungufu baada ya Fabian Delph kulimwa kadi nyekundu mwishoni kabisa mwa kipindi cha kwanza.

Matokeo hayo ya Manchester City ambayo ilipewa nafasi kubwa ya kushinda yamechukiza watu wengi ambao hushiriki michezo ya kubashiri na hii imetokana na ubora wa Manchester City msimu huu.

No comments

Powered by Blogger.