COASTAL NA KMC ZAPANDA LIGI KUU
Timu KMC ya Dar es Salaam na wagosi wa kaya Coastal
Union zote za kundi B zimeungana na JKT Ruvu kupanda ligi kuu ya Vodacom
Tanzania bara msimu wa 2018/2019 baada ya kuibuka na ushindi katika mechi za
mwisho zilizopigwa leo
KMC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Jktt
Mlale katika uwanja wa ugenini mkoani Songea
Bao pekee la Kmc limefungwa na Abdulhalim Humud
katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo na kudumu mpaka dakika 90
Mechi Nyingi iliokuwa yakusisimu ilikuwa kati ya
wagosi wa Tanga Coastal Union na Mawezi Market ya Morogoro mchezo uliofanyika
katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Wagosi wakaya wameibuka na ushindi wa mabao 2-0
dhidi ya Mawezi Market ya Morogoro na kufikisha pointi 26, mabao ya Coastal
yalifungwa na Raizan Hafidh na Athuman Idd 'Chuji'
KMC NA Coastal wameungana maafande wa JKT Ruvua
kupanda ligi kuu msimu ujao kutoka kundi A baada ya kufikisha pointi 34 wakiwa
na mechi moja mkononi.
Matokeo kamili ya mechi za FDL zilizochezwa leo
Mbeya Kwanza 3-1 Polisi Dar
Mufindi United 1-2 Polisi Tanzania
JKT Mlale 0-1 KMC
Mawenzi Market 0-2 Coastal Union
No comments