HARAMBEE STARS YATINGA FAINALI CHALENJI

Nusu fainali ya kwanza ya michuano ya kombe la Cecafa Chalenji imeisha kwa  wenyeji timu ya Kenya 'Harambee Stars' ikitinga Failnali ya michuano hiyo kwa kuifunga Burundi bao 1-0

Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya bila kufungana katika dakika 90 za kawaida kabla ya kwenda kwenye muda wa nyongeza.

Whyvonne Isuza alifunga bao hilo pekee katika dakika ya 94.

Kenya itakutana na mshindi kati ya mabingwa watetezi Uganda dhidi ya Zanzibar ambao watacheza kesho ikiwa nusu fainali ya Pili

No comments

Powered by Blogger.