CHELSEA MDOMONI MWA BARCELONA, REAL MADRID KUIVAA PSG RATIBA KAMILI HII HAPA

Image result for UCL DRAW
Ratiba kamili ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora imepangwa mchana huu Mjini Nyon Uswis ambapo mechi kali na za kuvutia zimeonekana kupangwa safari hii.

Mabingwa wa England klabu ya Chelsea wenyewe wamepangwa kukutana na moja kati ya timu zinazocheza soka la kuvutia na ngumu kuziondoa mashindanoni Barcelona mpambano unaotarajiwa kuvuta hisia za wengi hasa ikizingatiwa kwamba Chelsea ndiyo klabu pekee yenye rekodi nzuri dhidi ya Barcelona kutoka England.

Mechi nyingine inayoonekana kuvutia zaidi ni baina ya mabingwa watetezi wa kombe hilo Real Madrid ambao wamepangwa dhidi ya PSG toka Ufaransa. Mechi hii inatarajiwa kuwa kali hasa kwa kuangalia ubora wa kkosi cha PSG hivi sasa.

Manchester United wao wamepangwa kucheza dhidi ya Wawakilishi wa Hispania Sevilla katika hatua hii wakati vinara wa ligi kuu ya England Manchester City wao watacheza na FC Basel kutoka Uswisi.

RATIBA KAMILI HII HAPA


  • Real Madrid vs PSG
  • Chelsea vs Barcelona
  • Sevilla vs Manchester United 
  • FC Basel vs Manchester City
  • Shakhtar Donetsk vs Roma
  • Bayern Munich vs Besiktas
  • Juventus vs Tottenham Hotspur
  • Porto vs Liverpool
MECHI ZA AWALI ZITACHEZWA TAREHE 13/14 na 20/21 MWEZI FEBRUARI 2018 NA MECHI ZA MARUDIANO NI TAREHE 6/7 na 13/14 MWEZI MACHI 2018

1 comment:

  1. Acha Wafu Wazikane Halafu Sisi Tupite Hivi 🕴🕴 Kwa Mwendo Wa Kunyata..

    ReplyDelete

Powered by Blogger.