ARSENAL WAPANGWA NA WASWEDEN, DORTMUND YAPELEKWA ITALIA EUROPA LEAGUE

Image result for EUROPA LEAGUE LAST 32
Hatua ya 32 bora ya michuano ya Europa league imepangwa mara tu baada ya kumalizika kwa upangaji wa ratiba ya michuano ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Europa League michuano mikubwa namba mbili katika ngazi ya klabu ambapo bingwa wake atapata nafasi ya kucheza katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao inajumuisha timu 8 ambazo zimeshika nafasi ya 3 kwenye makund ya ligi ya mabingwa Ulaya pamoja na timu 24 zilizokua zikipambana kutaka kuvuka hatua ya makundi ya michuano hii.

Arsenal kutoka England ni moja ya jina kubwa kwenye michuano ya mwaka huu ikipangwa kucheza dhidi ya timu wawakilishi toka Sweden klabu ya Ostersunds huku Borusia Dortmund baada ya kutupwa nje katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya itabidi kukaza msuli walau kunyakua kombe hili ikipangwa kucheza dhidi ya Atalanta toka Italia klabu ambayo imeitupa nje Everton kwa kushinda mechi zote mbili.

HII HAPA RATIBA KAMILI 

  • Borussia Dortmund vs Atalanta
  • Nice vs Lokomotiv Moscow
  • Copenhagen vs Atletico Madrid
  • Spartak Moscow vs Athletic Bilbao
  • AEK Athens vs Dynamo Kiev
  • Celtic vs Zenit St Petersburg
  • Napoli vs Leipzig
  • Red Star Belgrade vs CSKA Moscow
  • Lyon vs Villarreal
  • Real Sociedad vs Salzbug
  • Partizan Belgrade vs Viktoria Plzen
  • Steaua Bucharest vs Lazio
  • Ludogorets vs AC Milan
  • Astana vs Sporting Lisbon
  • Ostersunds vs Arsenal
  • Marseille vs Braga 
RATIBA INAONYESHA MECHI ZITACHEZWA TAREHE 15 FEBRUARI 2018 NA MARUDIANO NI TAREHE 22 FEBRUARI 2017.


No comments

Powered by Blogger.