STARS KWENDA BENIN BILA SAMATTA
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) inayodhaminiwa na Bia ya
Serengeti, Mbwana Ally Samatta, atakosa mchezo kati Tanzania na Benin utakaofanyika
Novemba 12, 2017 kutokana na kuwa majeruhi.
Taarifa kutoka kwa matatibu wa Genk ya Ubelgiji,
zinasema kwamba Mbwana Samatta anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mdogo na mpaka
kupona, madaktari wamesema itamchukua wiki nane ili kurejea uwanjani.
Kocha wa Taifa Stars, Salum Shabani Mayanga
amepokea taarifa hiyo na kusema haijawa bahati kwa Stars, lakini atapanga
kikosi chake vema kwa wachezaji atakaokuwa nao huko Benin akiwamo Abdi Banda na
Farid Mussa.
Wachezaji watakaosafiri ni Aishi Manula, Peter
Manyika, Gadiel Michael, Boniphas Maganga, Kelvin Yondani, Nurdin Chona, Himid
Mao, Hamis Abdallah, Raphael Daudi, Mohamed Issa, Jonas Mkude, Mudathir Yahya,
Simon Msuva, Shiza Kichuya, Faridi Mussa, Ibrahim Ajib, Mbaraka Yusuph na
Elias Maguli.

No comments