KIPA NAMBA 1 SAUZI KUIKOSA SENEGAL KUFUZU KOMBE LA DUNIA

Itumeleng Khune kipa namba moja wa timu ya taifa ya Afrika Kusini  huenda akakosa michezo miwili muhimu ya kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia dhidi ya Senegal.
Khune mmoja ya makipa waliojijengea jina barani Afrika aliumia mfupa wa karibu na jicho la kulia wakati timu yake ya Kaizer Chief ilipocheza na Chippa United katika ligi kuu ya Afrika Kusini.
Taarifa kutoka Hospitali imeeleza kuwa Khune anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja mpaka wiki sita kama kutakuwa na haja ya kufanyiwa upasuaji lakini kuna tetesi zinasema kipa huyo huenda akaonekana langoni na imefanywa kuwa siri mazoezi yake ikiwa ni mbinu pia ya kuikabili Senegal
Afrika kusini watacheza na Senegal siku ya ijumaa katika mchezo wa kuwania kufuzu na ni lazima kushinda mchezo huo ili kupata nafasi ya kwenda Urusi mwakani.
No comments