MAN CITY YAPATA USHINDI WA JIONI, ROONEY APIGA GOLI LA "MWAKA" EPL JANA USIKU

Everton 4-0 West Ham: Wayne Rooney bags amazing hat-trick
Hatua ya 14 ya ligi kuu nchini England ilikamilishwa jana Usiku kwa mechi 6 kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini England macho ya wengi yalikuwa katika uwanja wa Etihad ambapo vinara manchester City walikua wakiikaribisha Southampton.

Manchester City ilibidi wasubiri mpaka dakika za lala salama kupata bao la ushindi na kuibuka na ushindi wa bao 2-1 goli la dakika ya mwisho ya muda wa nyongeza la mshambuliaji Raheem Sterling wengi wakiamini kama mchezo ungemalizika kwa sare ya bao 1-1 baada ya City kutangulia kufunga bao la kwanza kupitia kwa Kevin De Bryune kisha Southampton ikasawazisha kupitia kwa Oriol Romeu.

Katika mchezo mwingine hiyo jana Everton ilizinduka usingizini na kupata ushindi wa bao 4-0 dhidi ya West Ham huku Wayne Rooney akifunga mabao matatu huku goli moja likiwa ni bonge la Goli baada ya kupiga shuti toka katikati ya Uwanja na kwenda moja kwa moja goli. Goli lingine lilifungwa na beki Ashley Williams huku kocha mpya wa Everton Big Sam akishuhudia toka jukwaani.

Katika mechi nyingine Mabingwa watetezi Chelsea wakiwa nyumbani waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Swansea bao pekee la mlinzi wa pembeni Antonio Ruediger na kuendelea kung'ang'ania katika nafasi ya 3 wakifikisha pointi 29.

Burnley iliendeleza wimbi la ushindi msimu huu ikiibuka na ushindi wa bao 2-1 ugenini dhidi ya Bournemouth wakati Liverpool wao wakaifunga Stoke city bao 3-0 Mohammed Salah akifunga bao 2 na bao moja la Sadio Mane.

Arsenal wao wakiwa nyumbani waliifunga Huddersfield bao 5-0 habari ya mechi hii bofya hapa http://www.wapendasoka.com/2017/11/arsenal-yatoa-aonyo-kwa-man-united.html 

No comments

Powered by Blogger.