ARSENAL YATOA AONYO KWA MAN UNITED YAIADHIBU HUDDERSFIELD "MKONO"

Arsenal 5-0 Huddersfield: Match report
Siku chache kabla ya pambano la ligi kuu ya soka ya England baina ya Arsenal na Manchester United, Arsenal imetoa onyo kwa United kujipanga vyema baada ya kuifunga Huddersfield Town bao 5-0 moja kati ya mechi 6 za ligi kuu ya England zilizochezwa jana Usiku katika dimba la Emirates.

Olivier Giroud alifunga mabao mawili huku Alexandre Lacazette, Alexis Sanchez na Mesuit Ozil wote walifunga bao moja kila mmoja kukamilisha moja kati ya ushindi mkubwa kwa Arsenal msimu huu.

Matokeo hayo yanaifanya Arsenal kufikisha pointi 28 katika nafasi ya nne ikiwa ni pointi 1 nyuma ya Chelsea wenye pointi 29, pointi 4 nyuma ya United wenye pointi 32 na pointi 12 nyuma ya vinara Manchester City.

No comments

Powered by Blogger.