ALIYEKUA KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA WALES APEWA MIKOBA YA KUINUSURU SUNDERLAND
Aliyekua kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Jamhuri ya Wales Chris Coleman amekubali kuchukua jukumu la kuinoa klabu ya Sunderland ya Ligi daraja la Championship Nchini England
Sunderland ambayo ilishuka daraja msimu uliopita imejikuta ikishika mkia katika msimamo wa ligi hiyo daraja la Championship ambayo hutoa washindi watatu watakaocheza ligi kuu msimu ujao.
Coleman ambaye ameshindwa kuiongoza Wales kupata nafasi ya kucheza katika michuano ijayo ya kombe la dunia nchini Russia anakabiriwa na kibarua kigumu kuweza kuinusuri timu hiyo isishuke tena daraja kutoka daraja iliyopo ikiwa na matokeo mabaya sana hasa katika mechi zake za nyumbani ambapo haijawahi kushinda mchezo wowote.
Kocha huyo mwenye miaka 47 amesaini mkataba wa miaka 6 kuifundisha Sunderland na mtihani wake wa kwanza utakua Jumanne hii dhidi ya Aston Villa.
No comments